Simba yatinga fainali ya mapinduzi cup.
SIMBA SC ya jijini dar es salaam imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la mapinduzi baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Yanga pia ya dar es salaam kwa mikwsju 4-2,katka pambano gumu la nusu fainali,na sasa simbaitakutana na Azam iliyoshinda nusu fainali ya mapema kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya taifa ya jang'ombe.
Mchezo ulianza kwa kasi kila timu ikitafuta bao la mapema,lakini mpaka kipindi cha kwanza kinaisha hakukuwa na timu iliyopata goli licha ya kosa kosa za hspa na pale kwa timu zote mbili. Haruna niyonzima akikosa kwa upande wa yanga na mohamedi ibrahimu kwa upande wa simba.
Kipindi cha pili kilishuhudia mabadiliko kwa timu zote mbili,lakini si simba wala yanga iliyofanikiwa kupata bao mpaka dakika tisini zinakamilika. Ndipo ilipoamuliwa mikwaju ya penati iamue mshindi,ambapo simba walipata penati nne dhidi ya mbili za yangu.
Kwa upande wa simba wafungaji walikuwa no nahodha Jonas mkude,kipa Daniel Agyei,mwanjali akakosa,mdhamiru akafunga ya kwake huku bokungu akimalizia,penati ya ushindi. Kwa upande was yanga wafungali walikuwa ni Simon msuva,kamusoko huku penati za golikipa dida na beki haji mwinyi zikiota mbawa.
No comments:
Post a Comment